Kikomo au nukta (.)
Huonyesha sentesi imekamilika.Mfano
Mamake ameenda sokoni.
Kiulizi (?)
Hutumika kuuliza swali.Mfano
Ni mpira upi uliochezewa na watoto asubuhi?
Alama ya kipumuo / koma / Kituo (,)
Hutumika kwa njia zifuatazoa) Kugawanya sentensi ndefu na kumpa msomaji nafasi ya kupumua
MfanoTuliposafiri kwa saa nane, tulipumzika kidogo kisha tukaendelea na safari yetu.
b) Kuorodhesha mambo au vitu
MfanoTumeenda sokoni kununua nyanya, vitunguu, mboga na dania za kupikia wageni.
c) Kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo au kitu
MfanoBwana Kazungu, mwalimu mkuu wa shule yetu, ndiye mkuu wa Kiswahili.
Herufi kubwa
Herufi kubwa hutumika mwanzoni mwa sentensi, mwanzoni mwa jina la mtu au mji, nchi au mahali.Mfano
Mto Tana na Athi ndiyo mito mirefu zaidi nchini Kenya.
Kihisishi / mshangao / kimako (!)
Hutumika kuonyesha hisia tofauti kama vile; furaha, mshangao, hasira au huzuni.Mfano
Lo! unamshika nyoka.
Huree! tumeushinda uchaguzi kwa awamu nyingine.
Vidondozi / vinukuu / vinukulu (")
Hutumika kwa njia zifuatazo:a) Hutumiwa kuonyesha usemi halisi au maneno yalivyosemwa bila kuyabadilisha
Mfano"Endeni mchezee uwanjani," mwalimu aliwaeleza watoto.
b) Kuonyesha neno lisilo la kiswahili.
MfanoWatu wanapopika "chips" hutumia mafuta.
Mkwanju / Mkato (/)
Hutumika kuorodhesha mambo au maneno yenye maana sawa.Mfano
Magari ya matwana / matatu / daladala hutumika zaidi nchini kenya.
Dukuduku / vitone (...)
Huonyesha kuwa usemi haujakamilika ama kuna maneno ambayo hayajaandikwa.Mfano
Sitasema jambo lolote lakini ...
Koloni / nukta mbili (:)
Hutumika kwa njia zifuatazo:a) Hutumiwa kuonyesha usemi halisi au maneno yalivyosemwa bila kuyabadilisha
MfanoViungo vya mapishi vilivyo nunuliwa na mama vilikuwa: dania, masala, tangawizi na karafuu.
b) Katika uandishi wa mazungumzo
MfanoMwalimu: Mbona umechelewa kuingia darasani?
Koki: Samahani mwalimu, gari la kubebea wanafunzi limechelewa leo.
Nusu koloni / nukta mkato (;)
Hutumika kuonyesha sehemu ya pili inayoelezea zaidi kuhusu sehemu iliyotangulia.Mfano
Alionywa kwa kosa hili mara tatu; hajabadilika hata kidogo.
King'ong'o / ritifaa (')
Hutumika kukata neno ilikubadilisha sauti.Mfano
Ng'ombe huyu hula zaidi kila siku.
Mabano / Parandesi( )
Hutumiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo liIilosemwaMfano
Ezekiel Kemboi (mwanariadha mashuhuri) ameishindia Kenya dhahabu katika mashindano mablimbali duniani.
Kistari kifupi (-)
Hutumika kwa njia zifuatazo:a) Kusisitiza sauti
MfanoWalmcheka ha-ha-ha alipoingia darasani.
b) Kuunganisha tarakimu kuonyesha mwanzo hadi mwisho
MfanoAlikuwa naibu mwalimu mkuu kutoka 2013-2017.